1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW-YORK: 51 kufikishwa mahakama ya The Hague juu ya mzozo wa Darfur

6 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFPu

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa amewasilisha majina 51 mbele ya mahakama ya kimataifa ya mjini The Hague ya watuhumiwa wa uhalifu wa kivita katika eneo la Dafur.

Hatua hiyo imetajwa kuwa ya kwanza kuelekea kufunguliwa mashtaka kwa watuhumiwa hao.

Orodha hiyo ya majina 51 imetolewa baada ya Umoja wa Mataifa kufanya uchunguzi wake mwaka uliopita ambapo iliripotiwa kufanyika mauaji unajisi na kuchomwa moto vijiji katika eneo la Darfur.

Kesi hiyo ya Darfur ndio ya kwanza kuwahi kuwasilishwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa katika mahakama ya kimataifa ya mjini The Hague.

Waliotajwa katika Orodha hiyo ni pamoja na maafisa wa serikali ya Khartoum,viongozi wa kundi la wanamgambo wa kiarabu la Janjaweed pamoja na waasi.

Awali hapo jana tume ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa iliwasilisha katika mahakama hiyo stakabadhi muhimu kuhusiana na mzozo wa Darfur.

Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya watu laki moja na nusu waliuwawa na mamilioni ya wengine kuyahama maskani yao tangu kuanza mzozo huo wa miaka miwili.