1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW DELHI. Joto kali laua India.

18 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFCW

Serikali ya India imetoa taarifa ya kuuwawa kwa watu 18 kufuatia joto kali nchini humo siku chache zilizopita.

Lakini habari ambazo hazikuthibitishwa zinasema kuwa kuna uwezekano kuwa watu 130 huenda wakawa wamepoteza maisha kufatia kiwango cha joto kilichopanda na kufikia nyuzi 50.

Watalaamu wa kimatibabu wamesema kuwa vifo hutokea kutokana na mwili kukosa maji.

Hali kama hii iliwakumba zaidi watu masikini na wasio na makao nchini India mwaka 2003 ambako watu 1,400 walikufa kutokana na joto kali.