1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Netanyahu arejea madarakani nchini Israel

Kiswahili29 Desemba 2022

Benjamin Netanyahu ameidhinishwa kuwa Waziri Mkuu wa Israel hii leo baada ya baraza lake la mawaziri la mrengo mkali wa kulia kuapishwa.

https://p.dw.com/p/4LXz9
Benjamin Nentayahu kuongoza tena serikali ya mseto Israel
Benjamin Nentayahu kuongoza tena serikali ya mseto IsraelPicha: AMIR COHEN/REUTERS

Netanyahu, kiongozi mkongwe,mwenye miaka 73 aliefunguliwa mashtaka kwa tuhuma za ufisadi ambazo anakanusha, ametaka kutuliza wasiwasi kuhusu hatima ya haki za raia na diplomasia tangu kambi yake ya vyama vya utaifa na kidini vilipata wingi wa wabunge katika uchaguzi wa Novemba 1.

Netanyahu ameahidi mara kwa mara kukuza uvumilivu na kusaka amani. Aliambia bunge la Israel hii leo kwamba kumaliza migogoro baina ya Waisraeli-Waarabu ilikuwa kipaumbele chake kikuu, pamoja na kuzuia mpango wa nyuklia wa Iran na kujenga uwezo wa kijeshi wa Israeli.

''Kuendelea kupanua mzunguko wa amani na mataifa ya Kiarabu kwa lengo la kumaliza mzozo wa Waarabu na Israeli mara moja na kwa wote. Hii ni mara ya sita ninawasilisha serikali inayoongozwa nami kwa idhini ya Knesset, na nina furaha kama mara ya kwanza.",alisema Netanyahu.

Wapinzani walimkosoa wakisema Netanyahu alilazimika kufanya mikataba ya gharama kubwa ili kupata washirika wapya baada ya hapo vyama vya mrengo wa wastani vilimsusia kwa sababu ya matatizo yake ya kisheria.

Bunge la Israel, Knesset, laidhinisha serikali ya Netanyahu
Bunge la Israel, Knesset, laidhinisha serikali ya Netanyahu Picha: AMIR COHEN/REUTERS

Kwa Wapalestina, tayari wanamtazamo mbaya kuhusu sera ya Netanyahu, katika kupanua ujenzi wa makazi katika Ukingo wa Magharibi, eneo ambapo Wapalestina wanatarajia kujenga taifa lao la baadaye.

Mataifa mengi yenye nguvu duniani yanaona kuwa makazi yamejengwa kwenye ardhi iliyochukuliwa katika vita kinyume cha sheria. Nabil Abu Rudeineh, msemaji wa Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa sera za ujenzi ya Israel zitakuwa na athari kwa kanda hilo.

Netanyahu, ambaye sasa anaingia muhula wake wa sita, anasema atahudumumia Waisraeli wote. Netanyahu, ambaye alikuwa waziri mkuu kwa miaka kumi na mitano (1990-1993 na 2009 hadi 2021), amesema anatafuta mafanikio katika kuunda uhusiano wa kidiplomasia na Saudi Arabia kama alivyofanya mnamo 2020 na mataifa mengine ya Ghuba ambayo yanaunga mkono wasiwasi wa Israeli kuhusu Iran.

Saudi Arabia haijaashiria mabadiliko yoyote katika msimamo wake kuhusu ushirikiano na Israel ambao unategemea Palestina. Uteuzi wa Netanyahu ni pamoja na Itamar Ben-Gvir, kama waziri wa polisi. Ben-Gvir, mwanasheria, anasema hivi sasa mimisamo yake imekuwa ya wastani zaidi.

Wakati huohuo,waziri wa zamani Amir Ohana, kutoka chama cha Likud,amechaguliwa kuwa spika wa bunge la Israel, la Knesset.