1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Netanyahu aongezewa muda kuunda serikali mpya

9 Desemba 2022

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amepewa leo nyongeza ya siku kumi hadi Desemba 21, awe ameunda serikali mpya

https://p.dw.com/p/4Kjhn
Symbolbild I  Israel: Prime Minister Benjamin Netanyahu am Telefon
Picha: Koby Gideon/ZUMA/IMAGO

Muda wake wa awali ukiwa ulitarajiwa kumalizika siku ya Jumapili, Netanyahu aliomba muda wa wiki mbili unaoruhusiwa na sheria. Rais Isaac Herzog, alimpa siku 10 za ziada.

Netanyahu aliteuliwa kuiongoza Israel kufuatia ushindi wa mrengo wa kulia katika uchaguzi wa Novemba 1.

Amepata uungwaji mkono bungeni lakini bado hajakamilisha makubaliano ya muungano wa vyama ili kuunda serikali.

Vyama havijaafikiana kuhusu suala la kugawana madaraka.

Mazungumzo hayo yamechukua muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa, wakati Netanyahu akiungwa mkono tangu mwanzo na vyama vya mrengo wa kulia na vile vya kidini vinavyodhibiti viti 64 kati ya 120 vya Bunge la Israel.

Iwapo Netanyahu atashindwa kufikia makubaliano na vyama husika, Rais Herzog anaweza kumteua mjumbe mwengine wa Bunge kujaribu kuunda serikali. Vinginevyo, kutaitishwa uchaguzi mpya.