1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Israel limezingira makazi ya kiongozi wa Hamas

7 Desemba 2023

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema jana kwamba vikosi vya Israel viliyazingira makazi ya kiongozi wa Hamas Yehya Sinwar, yaliyoko katika katika jiji la Khan Younis, huko Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4ZrkF
Hamas und Fatah führen Gespraeche in Kairo
Kiomgozi wa Hamas katika eneo la Gaza, Chief Yehya Al-Sinwar Picha: Mohammed Salem/REUTERS

Hata hivyo amekiri kwamba bado hawakuwa na uhakika ikiwa kiongozi huyo alikuwemo nyumbani kwake.Israel inaamini kwamba baadhi ya viongozi wa Hamas, huenda wamejificha katika eneo hilo la kusini ama kwenye mahandaki yaliyotapakaa Gaza.Katika hatua nyingine, Katibu Mkuuwa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametumia kifungu cha 99 cha Mkataba wa Umoja huo, kupeleka ombi la moja kwa moja kwa Baraza la Usalama juu ya hali mbaya ya kibinaadamu katika Ukanda wa Gaza. Hii ni mara ya kwanza Guterres kutumia kifungu hicho ambacho hutumika kwa nadra, tangu alipoingia madarakani mwaka 2017