1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu aapa kulipa kisasi dhidi ya Wahouthi

Angela Mdungu
15 Septemba 2024

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema nchi yake itatoa adhabu kubwa kwa waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran walioishambulia Israel kwa kombora mapema Jumapili.

https://p.dw.com/p/4ke8W
Benjamin Netanyahu akizungumza na waandishi wa habari 13.07.2024
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuPicha: Nir Elias/Pool Photo/AP/picture alliance

Netanyahu ameyasema hayo katika kikao chake cha wiki na baraza la mawaziri na amesisitiza kuwa amedhamiria kufanya kila liwezekanalo kuwarudisha kwenye makazi yao watu waliolazimika kuhama Kaskazini mwa Israel kutokana na hali ya usalama.

Soma zaidi: Jeshi la Israel lazuia kombora la masafa marefu kutoka Yemen

Netanyahu ametoa onyo hilo kwa waasi wa Kihouthi  muda mfupi baada ya kundi hilo kuthibitisha kuwa ndiyo limehusika na shambulio la kombora lililofika katikati mwa Israel kwa mara ya kwanza. 

Soma zaidi: Wahouthi wa Yemen waapa kulipiza kisasi shambulizi la Israel Hodeida

Hayo yanajiri wakati jeshi la Israel limekiri leo kwamba kuna uwezekano mkubwa kuwa shambulio lake la anga katika Ukanda wa Gaza ndilo lililowauwa mateka watatu raia wa Israel mwezi Novemba mwaka uliopita. Miili ya mateka hao ilirejeshwa nchini Israel mwezi Desemba. Kamanda wa kundi la Hamas Ahmed Ghandour, aliuawa kwenye operesheni hiyo.