1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ndege ya uokozi kutoka Niger yatua Ufaransa

2 Agosti 2023

Ndege ya kwanza kati ya tatu zinazowasafirisha raia wa Ulaya, wengi wao wakiwa Wafaransa ambao wanahamishwa kutoka Niger, imetua mjini Paris mapema leo.

https://p.dw.com/p/4UfyU
Niger I Fluggäste vor dem internationalen Flughafen Diori Hamani in Niamey
Picha: AFP

Hayo yamejiri wiki moja baada ya mapinduzi ya kijeshi kumuondoa madarakani mmoja wa viongozi wa mwisho wanaoungwa mkono na nchi za Magharibi katika kanda ya Sahel inayokumbwa na uasi wa itikadi kali. Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ufaransa Catharine Colonna alisema kabla ya ndege hiyo kutua katika uwanja wa Charles de Gaulle kuwa kulikuwa na watu 262 kwenye ndege hiyo wakiwemo watoto kadhaa. Wakati huo huo, Mipaka ya Niger ya ardhini na angani na nchi tano jirani imefunguliwa tena. Ilifungwa baada ya jeshi la ulinzi wa rais kumuondoa madarakani Rais Mohamed Bazoum. Mmoja wa wanajeshi waasi alisema kwenye televisheni kuwa mipaka yake na Algeria, Burkina Faso, Libya, Mali na Chad imefunguliwa tena.