1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nchi zisizofungamana na upande wowote zimetoa mwito wa kufanyiwa mageuzi umoja wa mataifa

14 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF3m

Mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa umoja wa nchi zisizofungamana na upande wowote wameelezea umuhimu wa kufanyiwa marekebisho umoja wa mataifa.Taarifa iliyotangazwa mwishoni mwa mkutano huo mjini Doha imesema mageuzi ya umoja wa mataifa yatazidisha nguvu za taasisi hiyo ya kimataifa dhidi ya hatua za upande mmoja.Mawaziri wa mambo ya nchi za nje wameelezea upinzani wao dhidi maamuzi ya upande mmoja,matumizi ya nguvu,vitisho,shinikizo na hatua nyenginezo zinazokwenda kinyume na sheria za kimataifa.Mkutano wa Doha umezungumzia pia njia za kupambana na ugaidi.Mkutano huo wa kundi la nchi zisizofungamana na upande wowote umefanyika pembezoni mwa mkutano wa kundi la G77 na China mjini Doha.