1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Umoja wa Ulaya wakubaliana vikwazo vipya dhidi ya Urusi

21 Juni 2023

Nchi za Umoja wa Ulaya zimekubaliana leo kupitisha vikwazo vipya dhidi ya Urusi kuhusiana na vita nchini Ukraine. Hayo ni kwa mujibu wa ujumbe uliochapishwa kwenye ukurasa wa Twitter na ofisi ya rais wa Sweden.

https://p.dw.com/p/4Stfh
EU-Haushalt
Picha: Virginia Mayo/dpa/picture alliance

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa Umoja wa Ulaya umeridhia kupitia vikwazo dhidi ya raia wengine zaidi wa Urusi pamoja na mashirika kutokana na hatua yao ya kuunga mkono vita vya Urusi nchini Ukraine.

Hatua hiyo yadaiwa kusaidia kuzipa pigo zaidi harakati za vita za Urusi

Rais wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen ameikaribisha hatua hiyo akisema itasadia kuzipa pigo zaidi harakati za vita za rais Putin katika wakati ambapo kuna vikwazo vya usafirishaji. Makubaliano hayo yamefikiwa na wanadiplomasia mjini Brussels na yanasubiri kuidhinishwa na viongozi wa nchi za Umoja huo.