1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nchi za Kiarabu zasisitiza kuutatua wa mzozo wa Syria

20 Mei 2023

Viongozi wa nchi za Kiarabu wamethibitisha azma yao ya kuutafutia ufumbuzi mzozo wa Syria wakati wa mkutano wao wa kila mwaka ambao umefanyika nchini Saudi Arabia.

https://p.dw.com/p/4RbLd
Gipfel der Arabischen Liga | Syriens Präsident Baschar al-Assad trifft in Dschidda ein
Picha: SANA/REUTERS

Katika taarifa ya pamoja ya tamko la Jeddah, viongozi wa mataifa hayo wamekaribisha kurejea kwa ujumbe wa serikali ya Syria katika mikutano na kusema kuwa wanapaswa kuzidisha juhudi za kuisaidia Syria kutatua mzozo wake yenyewe.

Mwishoni mwa mkutano huo wa kilele, waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia, Mwanamfalme Faisal bin Farhan alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa nchi yake itafanya mazungumzo na washirika wake wa nchi za magharibi juu ya uhusiano na Syria.

Rais wa Ukraine Volodmyr Zelensky alifanya ziara ya kushutukiza kuhudhuria mkutano huo. Akizungumza katika mkutano huo, Zelensky amewashutumu baadhi ya viongozi wa mataifa ya Kiarabu kwa kupuuza matukio mabaya yanayosababishwa na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine,  na kuwatataka viongozi wa jumuiya hiyo kuviangalia vita hivyo kwa jicho la haki na ukweli.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Rais wa Syria Bashar Al-Assad ikiwa ni mara ya kwanza tangu afukuzwe uanachama kutoka jumuiya ya nchi za kiarabu kwa zaidi ya muongo mmoja uliopita.