1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nchi 185 zazindua mfuko wa ufadhili wa kulinda asili

Sylvia Mwehozi
25 Agosti 2023

Viongozi wa mazingira kutoka mataifa 185 jana walikutana mjini Vancouver, Canada na kuzindua mfuko wa ufadhili wa kusaidia uhifadhi wa kimataifa wa mazingira.

https://p.dw.com/p/4VYaq
Nyangumi
Uhifadhi na Vivutio: Nyangumi 60-70 wakikusanyika karibu na Albany huko Australia Magharibi.Picha: WA Department of Biodiversity/AFP

Viongozi wa mazingira kutoka mataifa 185 jana walikutana mjini Vancouver, Canada na kuzindua mfuko wa ufadhili wa kusaidia uhifadhi wa kimataifa wa mazingira. Umoja wa Mataifa umetoa wito wa ufadhili ili kufikia malengo ikiwa ni pamoja na kulinda asilimia 30 ya ardhi na maeneo ya pwani ifikapo mwaka 2030.

Canada iliyokuwa mwenyeji wa mkutano huo imeahidi kutoa dola milioni 147 za Kimarekani na Uingereza ikichangia dola milioni 12. Chini ya mpango huo, nchi zenye maendeleo duni na nchi za visiwa vidogo, zitapewa kipaumbele na kupokea zaidi ya theluthi moja huku asilimia 20 ikielekezwa kwenye miradi ya jamii ya watu wa asili.

Mkutano huo umefanyika miezi minane baada ya serikali kadhaa kukubaliana mfumo wa kimataifa wa Bioanuwaiambao unalinganishwa na Mkataba wa Paris wa kulinda mazingira.