1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO yakutana Bruxelles kuzungumzia suala la kutumwa wanajeshi zaidi nchini Afghanistan

13 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDCd

Maafisa wa ngazi ya juu wa jumuia ya kujihami ya magharibi NATO wanakutana kwa siri kushauriana namna ya kuimarisha vikosi vya kimataifa vya kulinda amani nchini Afghanistan vinavyoongozwa na NATO-ISAF.Katibu mkuu wa jumuia ya kujihami ya magharibi NATO,bwana Jaap de Hoop Schaeffer amezisihi nchi wanachama wawajibike zaidi ili kuweza kukabiliana na mashambulio yanayozidi ya waasi wa Taliban.Uturuki,Hispania,Italy na Ufaransa zinapinga fikra hiyo kutokana na wanajeshi wao kuwajibika kwengineko ulimwenguni.Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Condoleezza Rice ameonya akiwa ziarani nchini Canada dhidi ya kushindwa shughuli za ISAF nchini Afghanistan.Amesema hapo patazuka patashika na nchi hiyo itazidi kuvurugika.Baraza la mawaziri la Ujerumani limerefusha kwa mwaka mmoja shughuli za jeshi la Ujerumani Bundeswehr nchini Afghanistan.