1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO yajadili utayari wake wa silaha zake za nyuklia

17 Juni 2024

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya kujihami ya NATO Jens Stoltenberg amesema jumuiya hiyo iko katika mazungumzo ya kutoa silaha zaidi za nyuklia katika hifadhi yake na kuziweka tayari kufuatia kitisho kutoka China na Urusi.

https://p.dw.com/p/4h8QS
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya kujihami ya NATO Jens Stoltenberg
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya kujihami ya NATO Jens StoltenbergPicha: Dursun Aydemir/Anadolu/picture alliance / Anadolu

Stoltenberg amesema kuna majadiliano ya moja kwa moja kati ya wanachama wake kuwa na uwazi katika hifadhi yake ya silaha za nyuklia kutumiwa kama njia ya kujilinda.  

Katibu Mkuu huyo amesema lengo la NATO ni kuwa na dunia isiyokuwa na silaha za nyuklia lakini kama silaha hizi zipo, Jumuiya hiyo itabakia kuwa Jumuiya ya nyuklia kwa sababu dunia iliyo na mataifa kama Urusi, China na Korea Kaskazini zinazomiliki silaha hizo ni dunia iliyo hatari. 

Soma pia:NATO yajadili urasimishaji wa msaada kwa Ukraine

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameonya mara kwa mara kwamba huenda akatumia silaha hizo kujilinda dhidi mazingira magumu.