1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

NATO: Ukraine inapiga hatua katika uwanja wa mapambano

14 Juni 2023

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesema Ukraine inapiga hatua katika makabiliano yake dhidi ya Urusi na amebashiri kuwa viongozi wa NATO wataongeza msaada wa kijeshi kwa serikali ya Kyiv watakapokutana mwezi ujao.

https://p.dw.com/p/4SXp3
USA NATO Generalsekretär Jens Stoltenberg in Washington
Picha: Jonathan Ernst/REUTERS

Amesema msaada zaidi utatolewa katika mkutano wa kilele wa NATO utakaofanyika katikati ya mwezi Julai huko Vilnius, Lithuania.

Stoltenberg alitoa kauli hiyo alipokutana katika Ofisi ya Oval na Rais Joe Biden, ambaye alisema ahadi ya Marekani kwa NATO itasalia kuwa mwamba imara.

Stoltenberg amezuru Ikulu ya Marekani  huku kukiwa na maswali kama muhula wake katika kiti anachokalia utaongezwa au la. Kwa sasa anatarajia kuondoka mamlakani ifikapo Septemba baada ya kuongoza kwa miaka 9.