1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nani atakayemaliza nafasi ya 4 Bundesliga?

9 Mei 2022

Mbio za kuwania nafasi ya kushiriki mashindano ya Ulaya msimu ujao zimepamba moto. Baada ya mechi za mzunguko wa 33 zilizopigwa mwishoni mwa wiki iliyopita, RB Leipzig wanajikuta katika nafasi ya nne.

https://p.dw.com/p/4B2xM
Fußball Bundesliga RB Leipzig v FC Augsburg
Picha: Martin Rose/Getty Images

Leipzig wana pointi 57 halafu wanaowafuata ni SC Freiburg wenye pointi 55 kisha Union Berlin wao wako katika nafasi ya sita na pointi 54.

Ni nafasi moja tu ya kuwania kushiriki Champions League iliyosalia kwa kuwa Bayern Munich ambao ni mabingwa wameichukua nafasi ya kwanza huku ya pili ikichukuliwa na Borussia Dortmund na ya tatu wakijihakikishia Bayer Leverkusen.

Katika mechi ya mwisho Leipzig watakuwa wanacheza na Arminia Bielefeld kisha Freiburg wapambane na Bayer Leverkusen halafu Union Berlin wavaane na VfL Bochum mjini Berlin.