1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Namibia yaongeza hali ya tahadhari kufuatia ujangili wa faru

2 Aprili 2024

Serikali ya Namibia imezidisha tahadhari dhidi ya vitendo vya ujangili baada ya kutangaza kuwa faru 28 wameuawa na wawindaji haramu tangu kuanza kwa mwaka huu.

https://p.dw.com/p/4eL0Z
Faru kwenye mbuga ya Ufaransa
Faru na mwanawe kwenye mbuga moja magharibi mwa Ufaransa.Picha: picture alliance/dpa/MAXPPP

Wizara ya mazingira katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika imeeleza kuwa kumeitishwa mkutano wa dharura wa ngazi ya juu na maafisa wa usalama ili kupanga mikakati ya kukabiliana na wimbi la ujangili wa kikatili.

Mwaka 2022, faru 87 waliuawa kote nchini Namibia na takwimu za mwaka jana bado hazijatolewa.

Soma zaidi: Twiga katika hatari ya kutoweka

Mwishoni mwa mwaka huo wa 2022, kulikuwa na wastani wa faru 23,300 barani Afrika, na takriban faru 15,000 wanapatikana nchini Afrika Kusini.

Pembe za faruhung`olewa baada ya kuuawa na majangili ambao huziuza katika masoko ya barani Asia wanakozitumia katika madawa ya kienyeji.