1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI:Uchunguzi wa ubakaji washutumiwa

1 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFwO

Makundi ya kutetea haki za binaadamu yameshutumu uchunguzi uliofanywa na jeshi la polisi la Uingereza wa madai yaliotolewa na wanawake wa Kenya kwamba walibakwa na wanajeshi wa Uingereza waliokuwa mafunzoni nchini Kenya. Uchunguzi wa kina uliamuriwa kufanywa baada ya mamia ya wanawake wa Kenya kutowa madai hayo.Uingereza imesema baadhi ya madai yanaweza kuwa ya kweli lakini takriban repoti zote za polisi ya Kenya juu ya madai ya ubakaji yaliotokea miaka 30 iliopita zionaonekana kuwa sio za kweli.Makundi ya haki za binaadamu yamewashutumu wasaili kwa kutumia njia za kufadhaisha akili wakati wa kuwahoji wanawake hao Uingereza tayari imeamuriwa kulipa fidia ya mamilioni ya fedha kwa wananchi wa Kenya waliojeruhiwa kutokana na silaha zilizoachwa katika viwanja vya mazoezi katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.