1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI:Chama cha ODM chagawanyika vipande viwili

15 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBZ2

Chama kikuu cha upinzani nchini Kenya Orange Democratic Movement ODM-Kenya kimegawanyika kuwa makundi mawili ikiwa ni miezi mine kabla uchaguzi mkuu kufanyika mwishoni mwa mwaka.Vigogo wa chama hicho mbunge wa Langata Raila Odinga na Mwenzake wa Mwingi North Kalonzo Musyoka wanaongoza vyama viwili tofauti ODM na ODM-Kenya.

Bwana Odinga aliyekuwa mfungwa wa kisiasa na mwanawe was kiume mwanasiasa mkongwe wa zamani marehemu Oginga Odinga anaonekana kuchukua nafasi ya pili katika kura ya maoni.

Kalonzo Musyoka kwa upande wake ni waziri wa mambo ya nje wa zamani na mwanasheria anaonekana kuchukuia nafasi ya tatu katika kura hizo za maoni.

Kwa mujibu wa wadadisi wa kisiasa vigogo hao wawili walilazimika kuungana ili kuweza kupata ushindi katika uchaguzi ujao.Rais Mwai Kibaki aliye na umaarufu nchini humo kwa kuanzisha elimu ya bure na kusababisha ukuaji wa uchumi aliingia madarakani mwaka 2002 baada ya Daniel arap Moi kustaafu.Haat hivyo kiongozi huyo analaumiwa kwa kutopambana na rushwa na ufisadi vilevile miundo mbinu iliyo hali mbaya.