1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nairobi. WFP yapata makubaliano na maharamia walioiteka meli ya misaada ya umoja wa mataifa nchini Somalia.

6 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEnM

Mpango wa chakula wa umoja wa mataifa WFP , umesema leo kuwa makubalino yamefikiwa ili kuweza kuiacha huru bila masharti katika muda wa saa 72 , meli iliyokodishwa na umoja wa mataifa , ikiwa imebeba chakula cha msaada kwa wahanga wa maafa ya Tsunami nchini Somalia , ambayo ilitekwa nyara mwezi wa Juni.

Baada ya majadiliano ya muda mrefu, viongozi wa kikabila wa Somalia pamoja na viongozi wa mitaa kutoka katika eneo hilo ambalo meli hiyo imekamatwa tangu Juni 27 walikubaliana kwa niaba ya wateka nyara hao kuiachia meli hiyo, shehena yake pamoja na wafanyakazi katika muda wa siku tatu..

WFP pia imesema kuwa makubaliano yaliyofikiwa Ijumaa jioni sio hayaleti hakika ya kuachiwa kwa meli hiyo , lakini baada ya ahadi kadha kama hizo kutoka kwa wateka nyara hao hakuna kilichotokea.