1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI: Umoja wa mataifa walaani shambulio dhidi ya waziri mkuu wa Somalia

7 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEKx

Umoja wa mataifa umelilaani shambulio dhidi ya waziri mkuu wa Somali, Ali Mohammed Gedi, liliofanywa mwishoni mwa juma.

Bwana Gedi, aliponea chupuchupu katika jaribio la kutaka kumuua alipoutembela mji wa Mogadishu. Walinzi wake watano waliuwawa na maofisa wengine 12 wakajeruhiwa vibaya wakati msafara wake wa magari uliposhambuliwa kutumia silaha ndogo na makombora.

Mjumbe maalumu wa umoja wa mataifa nchini Somalia, Francois Fall, ametuma risala za rambirambi wka jamii za waathirwa wa shambulio hilo.