1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI: Meli ya umoja wa mataifa yatekwa nyara Somalia

13 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CESV

Waasi nchini Somalia wameiteka nyara meli ya pili ya umoja wa mataifa iliyokuwa imesheheni chakula. Wanamgambo sita waliivamia meli hiyo wakati ilipokuwa imetia nanga katika bandari ya Merka, yapata kilomita 100 kusini magharibi mwa mji wa Mogadishu.

Wafanyikazi wa meli hiyo, wakenya tisa na raia mmoja wa Uganda, walikuwa wakishukisha chakula kwenye bandari hiyo, ambacho baadye kingepelekwa kuwasaidia wasomali elfu 78 katika wilaya ya Jilib, kazkazini mwa Merka, ambayo imeathiriwa na machafuko, mafuriko, na ukosefu wa chakula.

Mkurugenzi wa shirika la chakula duniani nchini Somalia, Robert Hauser, amekilaani kitendo hicho.