1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NABANGA: Joseph Kony amewasili kusini mwa Sudan

17 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDBR

Kiongozi wa kundi la waasi wa Uganda,Joseph Kony amewasili katika kambi huru,kusini mwa Sudan kuambatana na makubaliano ya kumaliza mgogoro wa miaka 19.Mkuu wa tume ya waasi wa LRA inayofanya majadiliano,Martin Ojul amesema,Kony amewasili katika kambi ya Rikwangba iliyo kama yadi 550 kaskazini ya mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.