1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMyanmar

Myanmar yawaachia huru wafungwa 7,000 siku ya Uhuru

4 Januari 2023

Kiongozi wa kijeshi wa Myanmar, Jenerali Min Aung Hlaing, ameelezea mipango ya uchaguzi kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

https://p.dw.com/p/4Litx
Myanmar Naypyitaw | Militärparade
Picha: Aung Shine Oo/AP/picture alliance

Kwenye hotuba yake leo alipoliongoza taifa kuadhimisha miaka 75 ya uhuru wa taifa hilo, Hlaing ametoa wito wa umoja wa kitaifa.

Ameyahimiza mataifa, mashirika ya kimataifa na vilevile raia wake, kuunga mkono kile alichokitaja kuwa 'mfumo wa demokrasia ya vyama vingi unaoimarika kwa njia halisi' ambao utawala huo wa kijeshi umeelezea kuwa lengo lake.

Huenda hatua ya kwanza kamili kuelekea kuandaliwa kwa uchaguzi ikachukuliwa mwishoni mwa mwezi huu, wakati miezi sita iliyotangazwa kuwa ya dharura itakapomalizika.

Utawala huo umesema pia utawaachilia huru zaidi ya wafungwa 7,000, kuadhimisha miaka 75 ya uhuru wake kutoka kwa Uingereza.