1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe ashambuliwa

9 Juni 2020

Nchini Tanzania mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA na kiongozi wa kambi ya upinzani Freeman Mbowe, hapo jana ameshambuliwa na watu wasiojulikana wakati akirejea nyumbani kwake mjini Dodoma.

https://p.dw.com/p/3dUo5
Freeman Mbowe Oppositonsführer Tansania
Picha: DW/E. Boniphace

Nchini Tanzania mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA na kiongozi wa kambi ya upinzani Freeman Mbowe, hapo jana ameshambuliwa na watu wasiojulikana wakati akirejea nyumbani kwake mjini Dodoma.

Hili ni tukio la pili kutokea kwa viongozi waandamizi wa chama hicho baada ya shambulizi la risasi dhidi ya makamu mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu akiwa mjini Dodoma mnamo mwaka 2017.

Sikiliza kauli ya msemaji wa chama cha CHADEMA Tumaini Makene kuhusu shambulizi hilo.