1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwendesha mashtaka Ujerumani aonya juu ya kitisho cha ugaidi

19 Juni 2024

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa serikali Jens Rommel ametahadharisha juu ya kitisho cha ugaidi unaochochewa na itikadi kali za kidini akisema hilo ni moja ya masuala ya msingi ya kiusalama yanayoikabili Ujerumani.

https://p.dw.com/p/4hDxP
Vikosi vya usalama vya Ujerumani vikiwatawanya wanafunzi wanaounga mkono uhuru wa Wapalestina katika Chuo Kikuu cha Berlin Humboldt Ujerumani mnamo Mei 03, 2024.
Vikosi vya usalama vya Ujerumani vikiwatawanya wanafunzi wanaounga mkono uhuru wa Wapalestina katika Chuo Kikuu cha Berlin Humboldt Ujerumani mnamo Mei 03, 2024.Picha: Halil Sagirkaya/Anadolu/picture alliance

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa serikali Jens Rommel ameeleza kuwa kati ya matukio 700 ya uchunguzi uliofanyika mwaka uliopita kuhusu ugaidi na usalama wa serikali, karibu matukio 500 yalihusishwa na ugaidi unaochochewa na itikadi kali za kidini.

Ameongeza kuwa zaidi ya matukio 40 yalihusiana na uhalifu uliochochewa na siasa kali za mrengo wa kulia na matukio mengine matatu yalichochewa na itikadi kali za mrengo wa kushoto.

Soma pia: Hali ya usalama nchini Ujerumani bado ni tete, majasusi

Kadhalika, idadi ya matukio ya uhalifu yanayochochewa na siasa yameongezeka maradufu.

Mwendesha Mashtaka Mkuu huyo ametolea mfano wa tawi la kundi linalojiita Dola la Kiislamu la Khorasan na jinsi linavyoilenga Ujerumani kwa mashambulizi na kusajili wapiganaji wapya.