1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanariadha wa Uganda Benjamin Kiplagat auawa nchini Kenya

1 Januari 2024

Polisi nchini Kenya wanachunguza mauaji ya mwanariadha wa Uganda, Benjamin Kiplagat, ambaye mwili wake ulipatikana na majeraha ya visu ndani ya gari la kaka yake jana asubuhi viungani mwa mji wa Eldoret

https://p.dw.com/p/4am7M
Wanariadha wa Kenya katika mashindano ya mbio za Olimpiki mjini Tokyo nchini Japan mnamo mwaka 2020
Wanariadha wa Kenya katika mashindano ya mbio za Olimpiki nchini JapanPicha: LUCY NICHOLSON/REUTERS

Stephen Okal, kamanda wa polisi kutoka eneo la karibu la Moiben  amesema Kiplagat ameuawa, lakini hawajui nia yake kwa sasa.

Akiwa mkimbiaji wa mbio za masafa marefu, Kiplagat alibobea katika mbio za mita 3,000 za kuruka viunzi na maji. Aliiwakilisha Uganda katika mashindano sita ya Riadha ya Dunia na kwenye Olimpiki za Majira ya Kiangazi mnamo mwaka 2008, 2012 na 2016.

Afisa wa riadha nchini Kenya atoa wito wa kuharakishwa kwa uchunguzi

Afisa wa riadha nchini Kenya, Barnabas Korir, ameomboleza kifo cha mwanariadha huyo na kutoa wito kwa polisi kuharakisha uchunguzi na kuwachukulia hatua waliohusika.