1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanariadha Kipyegon wa Kenya ashinda mbio za mita 1500

23 Agosti 2023

Mwanariadha wa kike kutoka Kenya Faith Kipyegon ameshinda mbio za dunia za wanawake za mita 1500 na kutwaa medali yake ya tatu ya dhahabu kwenye mashindano yaliyofanyika Jumanne jioni mjini Budabest nchini Hungary.

https://p.dw.com/p/4VSvR
Mwanariadha wa Kenya Faith Kipyegon
Mwanariadha wa Kenya Faith Kipyegon Picha: Dylan Martinez/Getty Images

Mshindi huyo mara mbili wa Michezo ya Olimpiki alifukuza upepo kwa kasi ya kustaajabisha akiwaacha nyuma wanariadha wengine na kufanikiwa kuvuka mstari wa mwisho ndani ya dakika 3:54:87. 

Kipyegon anayeshikilisha  rikodi ya dunia ya mbio za mita 1500 alishinda medali zake mbili zilizotangulia mnamo mwaka 2017 na 2022. Vilevile anazo medali mbili za shaba alizoshinda mwaka 2015 na 019.

Kwenye mashindano ya hapo jana mwanariadha kutoka Ethiopia Diribe Welteji alinyakua medali ya shaba na Sifan Hassan wa Uholanzi alibeba medali ya fedha kwa kushika nafasi ya tatu.