1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

Mwanamfalme Harry wa Uingereza atarajiwa Mahakamani

5 Juni 2023

Mwanamfalme Harry wa Uingereza anatarajiwa wiki hii kufika Mahakamani ili kutoa ushahidi katika kesi yake dhidi ya mchapishaji wa Gazeti la udaku la Daily Mirror.

https://p.dw.com/p/4SCCR
London | Krönungsprozession von König Charles III. | Prinz Harry
Picha: Andy Stenning/REUTERS

Harry ambaye ni mtoto wa Mfalme Charles III, atakuwa katika kipindi cha miaka 130, mwanafamilia wa kwanza wa Ufalme wa Uingereza kutoa ushahidi mahakamani. Kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa leo au kesho.

Soma pia: Uamuzi wa Harry na mkewe Meghan waumiza familia ya kifalme

Kampuni ya Mirror Group imeshitakiwa na watu maarufu wapatao 100 kwa madai ya udukuzi wa simu na vitendo vingine vilivyo kinyume na sheria ambavyo vilitendeka kati ya mwaka 1991 hadi 2011.

Mwanzoni mwa kesi hiyo mwezi uliopita, Kampuni hiyo iliomba msamaha kwa tukio moja kuhusu Harryna kusema alikuwa na haki ya kulipwa fidia.