1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiIran

Mwanajeshi wa Iran awauwa wenzake watano kwa risasi

22 Januari 2024

Mwanajeshi mmoja amewashambulia kwa risasi na kuwauwa wenzake watano katika hospitali inayohudumia wanajeshi nchini Iran.

https://p.dw.com/p/4bWVL
Bunduki aina ya AK 47
Bunduki aina ya AK 47Picha: picture alliance / united archives

Shirika la habari la serikali ya Iran IRNA limeripoti kuwa, tukio hilo limetokea jana katika wilaya ya Kerman likimnukuu brigedia jenerali katika wilaya hiyo.

Kulingana na ripoti, mwanajeshi huyo aliingia katika hospitali inayohudumia wanajeshi na kuanza kufyatua risasi kiholela. Haikubanika mara moja lengo lake lilikuwa gani lakini alifanikiwa kutoroka.

Matukio kama hayo ni nadra sana kutokea nchini humo. Hivi karibuni, washambuliaji wawili wa kujitoa mhanga walijilipua na kuwaua karibu watu 100 katika wilaya ya Kerman.

Kundi linalojiita Dola la Kiislamu lilidai kuhusika na shambulio hilo.