1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanaharakati wa haki za mashoga aliyeuawa Kenya azikwa

17 Januari 2023

Mwanaharakati maarufu wa haki za waponzi wa jinsia moja nchini Kenya, ambaye maiti yake ilikutwa katika sanduku la chuma kandoni mwa barabara wiki iliyopita amezikwa nyumbani kwao magharibi mwa Kenya.

https://p.dw.com/p/4MKmY
Kenia Edwin Chiloba, LGBTQ Aktivist
Picha: Edwin Chiloba via Facebook/REUTERS

Kifo hicho cha Edwin Kiprotich Kipruto ambaye alijulikana zaidi kama Edwin Chiloba kimelaaniwa na marafiki zake pamoja na wanaharakati wa ndani na nje ya Kenya, wakitaka haki ichukue mkondo wake. Mamia ya watu walikusanyika kwenye nyumba ya familia yake kwenye kijiji cha Sergoit katika kaunti ya Elgeyo Marakwet, yapata kilomita 300 kaskazini magharibi mwa mji mkuu, Nairobi.

Kabla ya kifo chake, marehemu ambaye alikuwa na umri wa miaka 25 alikuwa muhanga wa mashambulizi ya mtandaoni. Joel Onteri aliyesoma shule moja na Edwin, ameomba udhalilishaji dhidi ya marehemu ukomeshwe, kwani licha ya yote yanasemwa juu yake anayo familia ambayo haipaswi kunyanyapaliwa.