1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Mwanafunzi wa miaka 14 awaua wenzake kwa bunduki Marekani

Sylvia Mwehozi
5 Septemba 2024

Watu wanne wameuawa baada ya mwanafunzi mwenye umri wa miaka 14 kufyatua risasi katika shule ya sekondari huko Gerogia nchini Marekani.Waliouawa wametambulika kuwa ni wanafunzi wawili na walimu wawili.

https://p.dw.com/p/4kHvw
Georgia | Marekani
Maafisa wa usalama wakiwa wamefika kwenye shule kulipofanyika shambulio la bunduki Georgia, MarekaniPicha: ABC Affiliate WSB/REUTERS

Watu wanne wameuawa baada ya mwanafunzi mwenye umri wa miaka 14 kufyatua risasi katika shule ya sekondari huko Gerogia nchini Marekani na kusababisha wanafunzi kukimbia hovyo wakitafuta mahali salama pa kujificha madarasani na kwenye uwanja wa mpira. Waliouawa wametambulika kuwa ni wanafunzi wawili na walimu wawili huku watu wengine tisa wakikimbizwa hospitali baada ya kujeruhiwa. Mshukiwa huyo ambaye ni mwanafunzi wa shule hiyo alijisalimisha mara moja na kuwekwa chini ya ulinzi.

Soma: Kijana mmoja amewafyatulia risasi wanafunzi na kuua mmoja na kuwajeruhi wengine nchini Marekani

Kijana huyo aliwahi kuhojiwa na shirika la upelelezi la Marekani FBI baada ya kupokea taarifa kutoka kwa mtu asiyejulikana mnamo Mei mwaka 2023 kuhusu vitisho vya mtandaoni vya kufanya ufyatuaji risasi shuleni. Wagombea urais Kamala Harris na Donald Trump wote wameeleza kusikitishwa na tukio hilo la mauaji.