1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSenegal

Waziri wa Ujerumani Baerbock aanza ziara Afrika Magharibi

16 Julai 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock ameanza ziara yake Afrika Magharibi katika taifa la Senegal.

https://p.dw.com/p/4iMLs
Baerbock ziarani Afrika Magharibi
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock aliwasili Dakar kituo chake cha kwanzaPicha: Britta Pedersen/dpa/picture alliance

Ziara hiyo ni juhudi za kuongeza ushirikiano wa Ujerumani na mataifa ya Afrika Magharibi, ili kuzuia kuenea kwa ukosefu wa usalama kunakoshuhudiwa kwa sasa katika mataifa ya Sahel. 

Soma pia: Baerbock aiangazia Sudan katika ziara yake ya Afrika Mashariki

Akizungumza mjini Dakar, Baerbock amesema usalama wa Afrika Magharibi na maendeleo ya siku zijazo ni mambo yenye uhusiano wa karibu na usalama na maendeleo ya Ulaya. Waziri huyo wa mambo ya nje wa Ujerumani amedai kwamba matatizo yanayoikabili Afrika magharibi kama ugaidi, uhamiaji, uhalifu na umaskini yanaiathiri pia Ulaya moja kwa moja.

Soma pia: Baerbock akutana na kiongozi wa kijeshi wa Mali

Ziara hii ya Baerbock inajiri wakati kukiwa na wimbi la ukosefu wa usalama katika eneo la Sahel. Baerbock atakuwa nchini Ivory Coast, nchi ambayo pamoja na Senegal, zinachukuliwa kama washirika wawili wakuu zaidi wa Ulaya, wakati ambapo mataifa mengi zaidi ya ukanda huo yanaigeukia Urusi kama mshirika.