1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAfghanistan

Mvua yasababisha vifo vya watu 15 Afghanistan

26 Mei 2024

Mvua kubwa inayoendelea kunyesha nchini Afghanistan imesababisha vifo vya watu 15 wakiwemo watu 10 wa familia moja kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4gI9D
Raia wa Afghanistan wameketi karibu na nyumba zilizoharibiwa na mafuriko katika wilaya ya Burka
Raia wa Afghanistan wameketi karibu na nyumba zilizoharibiwa na mafuriko katika wilaya ya BurkaPicha: Atif Aryan/AFP/Getty Images

Mvua kubwa inayoendelea kunyesha nchini Afghanistan imesababisha vifo vya watu 15 wakiwemo watu 10 wa familia moja kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Familia hiyo, inayojumuisha wazazi na watoto wao wanane, wanaripotiwa kupoteza maisha eneo la Faizabad, mji mkuu wa mkoa wa Badakhshan.

Soma pia: Watu 84 zaidi wapoteza maisha Afghanistan kwa mafuriko

Mkurugenzi wa idara ya kukabiliana na majanga katika mkoa huo Mohammad Akram amesema timu ya uokoaji imefanikiwa kuupata mwili wa mama pekee.

Mafuriko na mvua zimesababisha uharibifu mkubwa ikiwemo maafa ya mamia ya watu katika sehemu nyingi ya nchi hiyo ya bara Asia.

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa limetahadharisha kuwa manusura wanakabiliwa na hali mbaya ya kibinadamu.