1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Muungano wa upinzani Mali wataka uchaguzi haraka

2 Aprili 2024

Muungano wa zaidi ya vyama 80 vya siasa na makundi ya kiraia nchini Mali wameungana kutoa tamko la pamoja la kutaka uchaguzi wa rais ufanyike haraka iwezekanavyo.

https://p.dw.com/p/4eKte
Rais wa mpito wa Mali,  Assimi Goita.
Rais wa mpito wa Mali, Assimi Goita.Picha: Vladimir Smirnov/ITAR-TASS/IMAGO

Muungano wa zaidi ya vyama 80 vya siasa na makundi ya kiraia nchini Mali wameungana kutoa tamko la pamoja la kutaka uchaguzi wa rais ufanyike haraka iwezekanavyo ili kusitisha utawala wa mpito unaoongozwa na jeshi tangu mapinduzi ya mwaka 2020 na 2021.

Muungano huo umesema ikiwa tarehe mpya ya uchaguzi haitotangazwa, watatumia njia zote za kisheria kulifanikisha hilo.

Soma zaidi: Mali, Niger, Burkina Faso wanakabiliwa na uasi wa jihadi kwa muda mrefu

Mwezi Juni mwaka 2022, serikali ya kijeshi inayoongozwa na Kanali Assimi Goita iliahidi kurejesha mamlaka kwa raia mnamo Machi 26 mwaka huu  baada ya kufanyika uchaguzi wa rais mwezi Februari.

Hata hivyo, uchaguzi huo uliahirishwa na hadi sasa utawala wa kijeshi haujaelezea nia yake kuhusu mustakabali wa taifa hilo linalokabiliwa na uasi wa makundi ya kigaidi.