1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Muuguzi aliyewauwa watoto 7 ahukumiwa maisha.

21 Agosti 2023

Muuguzi wa kike aliyewaua watoto saba wachanga na kujaribu kuwauwa wengine sita, amehukumiwa kifungo cha maisha jela nchini Uingereza.

https://p.dw.com/p/4VPt4
UK Lucy Letby
Picha: Cheshire Constabulary/AFP

Jaji wa mahakama ya Manchester, kaskazini mwa England, ametowa hukumu hiyo dhidi ya Lucy Letby, mwenye umri wa miaka 33. Kesi hiyo imezusha ghadhabu kubwa kutoka upande wa familia za watoto wachanga waliouwawa, ambazo zilikataa kuhudhuria kikao cha kutowa hukumu hiyo, kitendo ambacho kimewafanya wanasiasa kuahidi kuziba mwanya wa kisheria katika matukio ya aina hiyo.Wengi wa watoto waliouliwa na Lucy Letby, aliyekuwa akifanya kazi katika hospitali ya Chester, walikufa kutokana na maumivu makali ya dawa alizokuwa akiwadunga.Muuguzi huyo aliweza kuyaficha mauaji hayo kwa kutowa taarifa za uwongo kuhusu alichokuwa akiwafanyia watoto hao.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW