1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMalawi

Mutharika aidhinishwa kugombea tena urais mwakani

19 Agosti 2024

Chama kikuu cha upinzani nchini Malawi cha Democratic Progress kimemuidhinisha hapo jana rais wa zamani Peter Mutharika kuwa mgombea wake katika uchaguzi wa rais mwaka ujao.

https://p.dw.com/p/4jcYj
Rais wa zamani wa Malawi Peter Mutharika
Mutharika atapambana na Rais wa sasa Lazarus Chakwera wa chama cha Malawi Congress anayewania muhula wa pili.Picha: picture-alliance/AP Photo/T. Chikondi

Mutharika mwenye umri wa miaka 84, ambaye alikuwa rais kuanzia mwaka 2014 hadi 2020, amesema katika hotuba yake kwamba yeye na chama chake watarekebisha hali ya kiuchumi, ambayo imeshuhudia ukuaji mdogo na uhaba wa sarafu za kigeni vilivyosababisha ukosefu wa mafuta na dawa.

Mutharika atapambana na Rais wa sasa Lazarus Chakwera wa chama cha Malawi Congress anayewania muhula wa pili katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Septemba 16, 2025.