1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Muendesha mashitaka: Washukiwa wa M23 wahukumiwe kifo

Josephat Charo
30 Julai 2024

Mwendesha mashataka nchini Congo amependekeza hukumu ya kifo kwa washtakiwa 25 wanautuhumiwa kwa kuwa wanachama wa kundi la waasi la M23 katika kesi inayoendelea mjini Kinshasa.

https://p.dw.com/p/4itwr
DR Kongo Kibumba 2022 | Waas wa M23
Waasi wa M23 wakiwa na silaha zao huko Kibumba, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Desemba 23, 2022.Picha: Moses Sawasawa/AP Photo/picture alliance

Afisi ya mwendesha mashtaka imetaka hukumu ya miaka 20 jela kwa mshukiw amwingine wa 26. Kundi la M23 linaoongozwa na Watutsi na kuungwa mkono na Rwanda limeyateka maeneo makubwa ya ardhi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo tangu mwishoni mwa 2021. Ni washukiwa watano tu ambao si maarufu kati ya wote walioshtakiwa, wanaohudhuria kesi hiyo katika mahakama ya kijeshi, huku wengine wakiwa hawajulikani walikojificha. Wanakabiliwa na mashitaka ya uhalifu wa kivita, kushiriki katika uasi na uhaini. Wawili wamekiri ni wanachama wa vuguvugu la kisiasa na kijeshi la makundi ya waasi la Alliance Fleuve Congo (AFC) lilioundwa Desemba mwaka jana mjini Nairobi Kenya na mwenyekiti wa zamani wa tume ya uchaguzi Corneille Nangaa, ambalo M23 ni mwanachama. Nangaa ni miongoni mwa washukiwa watano mashuri katika kesi hii wakiwemo pia rais wa kundi la M23 Bertrand Bisimwa, mkuu wa majeshi Sultani Makenga na msemaji Willy Ngoma na Lawrence Kanyuka.