1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Muasi wa zamani Niger aanzisha vuguvugu la kupinga mapinduzi

9 Agosti 2023

Kiongozi wa zamani wa waasi na mwanasiasa Niger amezindua vuguvugu linalopinga jeshi lililotwaa madaraka kupitia mapinduzi ya kijeshi ya Julai 26. Hiyo ni hatua ya kwanza ya upinzani wa ndani kwa utawala wa kijeshi Niger

https://p.dw.com/p/4Uxy9
Nach dem Militärputsch im Niger - Protest im Stadion
Picha: AFP

Rhisa Ag Boula amesema katika taarifa leo kuwa Baraza lake jipya la Upinzani kwa ajili ya Jamhuri - CRR linalenga kumrejesha madarakani Rais Mohamed Bazoum, ambaye amekuwa kizuizini nyumbani kwake tangu mapinduzi hayo.

Taarifa hiyo imesema Vuguvugu la CRR linaunga mkono Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi - ECOWAS na wahusika wengine wowote wa kimataifa wanaotaka kurejesha utaratibu wa kisheria nchini Niger.

Utawala wa kijeshi Niger wamzuia Mwanadiplomasia wa Marekani kumuona Bazoum

Ajuri Ngelale ni msemaji wa Rais wa Nigeria Bola Tinubu ambaye ndiye mwenyekiti wa ECOWAS, amesema Rais Tinubu akiwakilisha msimamo wa pamoja wa wakuu wa mataifa ya ECOWAS, amewasiliana kwa uwazi kuwa yeye pamoja na wenzake katika jumuiya hiyo wanapendelea suluhisho ambalo litapatikana kupitia njia za kidiplomasia, kupitia njia za amani, badala ya njia nyingine ile, na huo ndio utakuwa msimamo utakaodumishwa katika kwenda mbele, ukisubiriwa uamuzi mwingine wowote ambao huenda ukatoka au usitoke kwa mkutano wa kilele wa ECOWAS wa Alhamis. 

Watawala wapya wa kijeshi Niger wamekataa kukutana na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Kiuchumi ya ECOWAS.