1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
AfyaAfrika Kusini

Mtu mmoja afariki dunia kufuatia homa ya nyani Afrika Kusini

12 Juni 2024

Mlipuko wa homa ya nyani umesababisha kifo cha mtu mmoja na wengine 4 kuambukizwa huko Afrika Kusini. Haya yamesemwa na serikali ya nchi hiyo iliyodai kwamba inajaribu kununua dawa zaidi za kuutibu ugonjwa huo.

https://p.dw.com/p/4gy5J
Mtu mmoja afariki dunia baada ya kuugua homa ya nyani Afrika Kusini
Mtu mmoja afariki dunia baada ya kuugua homa ya nyani Afrika KusiniPicha: Institute of Tropical Medicine/dpa/picture alliance

Kulingana na waziri wa afya Joe Phaahla, visa hivyo vitano vilivyoripotiwa kati ya Mei 8 na Juni 7 ndivyo vya kwanza kurekodiwa nchini humo tangu mwaka 2022.

Homa ya nyani ni ugonjwa unaosababishwa na kirusi na unasambazwa kupitia mawasiliano ya karibu na mtu au mnyama aliyeambukizwa.

Mwaka 2022, maambukizi ya ugonjwa huo yaliongezeka kote duniani, hasa miongoni mwa wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja hatua iliyopelekea Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO, kutangaza hali ya dharura duniani.

WHO ilitangaza mwisho wa hali hiyo ya dharura mwaka jana ila maambukizi ya machache yanaendelea chini kwa chini.