1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mtoto wa Rusesabagina akosoa hukumu ya baba yake

20 Septemba 2021

Mtoto wa kike wa Paul Rusesabagina amekosoa uamuzi wa mahakama ya Rwanda kumkuta baba yake na hatia ya ugaidi.

https://p.dw.com/p/40ZYM
Ruanda | Kigali | Paul Rusesabagina zur Anhöhrung vor Gericht
Picha: Clement Uwiringiyimana/REUTERS

Carine Kanimba amesisitiza kuwa hukumu hiyo imetolewa kutokana na maamuzi ya Rais Paul Kagame.

Carine ameliambia shirika la habari la Ufaransa, AFP kwamba majaji wameamua kile ambacho Kagame alikitaka waamue na kwamba walitegemea hivyo.

Majaji bado wanaendelea kupitia idadi ya mashtaka mengine dhidi ya Rusesabagina na watuhumiwa wengine 20.

Hukumu dhidi yake inatarajiwa kutangazwa muda wowote leo.

Waendesha mashtaka wa Rwanda wametaka Rusesabagina, shujaa ambaye simulizi yake ilihamasisha filamu iliyopewa jina ''Hotel Rwanda'' ahukumiwe kifungo cha maisha jela.

Rusesabagina, mwenye umri wa miaka 67 aliyesaidia kuwaokoa maelfu ya watu katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, anashtakiwa kwa makosa tisa ikiwemo kuwa mwanachama wa kundi la kigaidi, kufadhili ugaidi, mauaji na ujambazi wa kutumia silaha.