1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mto Logone wavunja rikodi ya miaka 30 kwa kufurika

10 Oktoba 2024

Mto Logone umeanza kufurika kwa kiwango kikubwa kabisa kuwahi kushuhudiwa kwa zaidi ya miaka 30 illiyopita, ukitishia kuongeza hali mbaya inayoliandama taifa la Chad kwa wiki kadhaa sasa.

https://p.dw.com/p/4lbT4
Mafuriko nchini Chad.
Mafuriko nchini Chad.Picha: Abdullaue Adem/AA/picture alliance

Taarifa ya serikali imesema kwamba kufikia asubuhi ya jana, Jumatano, maji ya mto huo yalishafikia ukubwa wa mita 8.18, kiwango ambacho hakijafikiwa kwa miongo mitatu sasa.

Soma zaidi: Chad yatoa tahadhari ya mafuriko mabaya zaidi

Waziri Mkuu Allah Maye Halina amekutana na kamati ya usimamizi wa mafuriko kukubaliana juu ya mpango wa kukabiliana na janga hilo la kimaumbile, ambalo limezikumba wilaya nane kati ya kumi za mji mkuu, N'Djamena, na majimbo 17 kati ya 23 ya Chad.

Ofisi ya Uratibu wa Huduma za Kibinaadamu ya Umoja wa Mataifa inasema raia milioni 1.9 wa Chad wameathirika na mafuriko hayo.