1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaRwanda

Mshukiwa wa mauaji ya Kimbari ya Rwanda, mahakamani

10 Mei 2023

Mshukiwa wa mauaji ya kimbari ya Rwanda aliyekimbilia Ufaransa baada ya mauaji hayo ya mwaka wa 1994 na kuanza maisha mapya chini ya utambulisho bandia atafikishwa mahakamani leo.

https://p.dw.com/p/4R8eG
Pichani ni baadhi ya mafuvu ya wahanga wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda.
Mauaji ya kimbari nchini Rwanda mnamo mwaka 1994 yalihusisha watu kuuawa kwa kukatwakatwa mapanga.Picha: Ben Curtis/AP/picture alliance

Philippe Hategekimana, mwenye umri wa miaka 66 ambaye alipata uraia wa Ufaransa chini ya jina la Philippe Manier, atashitakiwa katika mahakama ya Paris kwa mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya ubinaadamu. Atakuwa mtu wa karibuni kabisa kufunguliwa mashitaka nje ya nchi kuhusiana na mauaji ya karibu watu 800,000. Hategekimana anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya Watutsi na pia kuweka vizuizi barabarani ili kuwazuia Watutsi ambao baadae waliuawa katika mkoa wa kusini wa Nyanza, ambako alifanya kazi kama afisa mwandamizi wa polisi. Amekanusha madai hayo. Hiyo ni kesi ya tano ya aina hiyo nchini Ufaransa kuhusiana na mauaji ya kimbari Rwanda.