1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Mshauri wa Macron aituhumu China kupeleka silaha Urusi

22 Julai 2023

Mshauri wa diplomasia wa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema China inapeleka vifaa vinavyoweza kutumiwa na Urusi kama zana za kijeshi.

https://p.dw.com/p/4UGiM
Frankreich | Emmanuel Bonne, der diplomatische Berater des französischen Präsidenten Emmanuel Macron
Picha: Stevens Tomas/Abacapress/IMAGO

Mshauri huyo wa Macron, Emmanuel Bonne amesema zana hizo huenda zikatumiwa na Moscow katika vita vyake dhidi ya Ukraine.

Aliyasema hayo katika hotuba yake ya nadra aliyoitoa katika Jukwaa la usalama la Aspen mjini Colorado. Ameeleza kuwa kwa wakati huu ambapo mashambulizi yanajibiwa kwenye uwanja wa mapambano, China inahitaji kuepuka kupeleka silaha Urusi.

Soma pia: Shambulio la droni laitikisa Crimea, ghala la silaha lalipuka

Ameiasa China kuonesha kuwa mshirika wa kuaminika katika mzozo wa Ukraine na kusisitiza kuwa ingawa hana ushahidi kwa sasa haamini kama China itatoa suluhisho katika mzozo huo.