1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAfrika

Msalaba Mwekundu waitisha misaada zaidi kwa wahitaji Morocco

12 Septemba 2023

Shirika la Msalaba Mwekundu limetoa wito wa msaada wa zaidi ya dola milioni 100 ili kuwasaidia wahanga wa tetemeko kubwa la ardhi nchini Morocco, lililosababisha vifo vya karibu watu 2,900.

https://p.dw.com/p/4WF2X
Shughuli za uokoaji zikiendelea Marrakesh Morocco
Shughuli za uokoaji zikiendelea Marrakesh MoroccoPicha: Said Echarif/AA/picture alliance

Mkurugenzi wa oparesheni katika shirika la kimataifa la msalaba mwekundu na hilali nyekundu IFRC Caroline Holt amesema wanasaka dola za kimarekanimilioni 112 ili kukidhi mahitaji muhimu kwa wakati huu.

Ameeleza kuwa, fedha hizo zinahitajika kwa ajili ya maji, usafi, vifaa vya msaada na mahitaji mengine ya kimsingi. 

Soma pia:Tetemeko la ardhi Morocco: Idadi ya waliokufa yafikia 2,681

Bi Holt amesema kuwa, wanafanya kila liwezekanalo ili kuepusha wimbi la pili la maafa.

Timu za uokoaji kutoka Morocco na nyengine kutoka nje ya nchi zinaendelea na shughuli za uokoaji na kutafuta manusura japo kuna dalili ndogo za kupata manusura zaidi.