1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MSAKO WA WANAMGAMBO NA SILAHA:

19 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFrI
BAGHDAD: Mwanajeshi mmoja wa Marekani ameuawa siku ya Alkhamis katika shambulio la ghafla pembezoni mwa barabara mjini Baghdad.Kwa upande mwingine wanajeshi wa Marekani kwa siku tatu kwa mfululizo wamesambaa katika mji wa Samarra kiasi ya kilomita 100 kaskazini mwa Baghdad,wakiwasaka wapiganaji wa chini kwa chini na silaha.Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Marekani wapiganaji wawili wa chini kwa chini wameuawa na wengine 86 wamekamatwa.