1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Msaada zaidi wa chakula wahitajika nchini Zimbabwe

Sylvia Mwehozi
7 Agosti 2019

Shirika la chakula la Umoja wa Mataifa limetoa rai ya kuomba msaada wa kiasi cha dola milioni 331, kwa ajili ya mamilioni ya Wazimbabwe wanaokabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula baada ya ukame mbaya.

https://p.dw.com/p/3NUwx
Simbabwe Nahrungsmittelhilfe
Picha: Privilege Musvanhiri

Shirika la chakula la Umoja wa Mataifa limetoa rai ya kuomba msaada wa kiasi cha dola milioni 331, kwa ajili ya mamilioni ya Wazimbabwe wanaokabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula baada ya ukame mbaya. Shirka hilo, WFP limesema takriban watu milioni 5, karibu theluthi moja ya watu wote milioni 16 wa Zimbabwe wanahitaji msaada wa chakula. Mkuu wa WFP David Beasley amesema Wazimbabwe milioni 2.5 wanakumbwa na hatari ya kufa njaa, na wengine milioni 5.5 watakuwa katika hali kama hiyo siku za usoni. Serikali inasema hali hiyo imesababishwa na hali mbaya ya hewa, lakini wakosoaji wanasema ni matokeo ya sera mbaya ya ardhi. Msimu wa kilimo uliopita ulikuwa mbaya sana, kutokana na ukame uliosababishwa na ukame wa el-Nino. Mssada ulioombwa na Umoja wa Mataifa unanuia pia kuwafaa wahanga wa vimbunga vilivyozikumbwa nchi kadhaa za Kusini mwa Afrika mapema mwaka huu, Zimbabwe ikiwemo.