1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MSAADA WA DHARURA KWA WAKIMBIZI:

14 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFjS

CAIRO: Shirika la Umoja wa Mataifa-Mpango wa Chakula Duniani(WFP)limetoa muito wa kupewa Dolla milioni 11 ili kuweza kuwasaidia kwa dharura maelfu ya wakimbizi wa Kisudani wanaoishi kambini nchini Chad.Wakimbizi hao wameyakimbia mapigano yanayozidi kushika kasi katika eneo la Darfur magharibi mwa Sudan.