1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MSAADA WA CHAKULA KWA KOREA KASKAZINI:

25 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFpi

WASHINGTON: Wizara ya kigeni ya Marekani imetangaza kuwa itapeleka Korea ya Kaskazini tani 60,000 za chakula ili kuzuia njaa na ukosefu wa chakula.Kwa mujibu wa msemaji Richard Boucher uamuzi huo umepitishwa kuambatana na ripoti za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mipango ya chakula duniani-WFP kuwa kiasi Wakorea Kaskazini milioni 4 wamo katika hali mbaya na wanahitaji msaada.Serikali ya Bush imesema mahitajio ya kiutu ya Korea ya Kaskazini hayachanganywi na ile hali ya kutofahamiana na serikali ya Korea ya Kaskazini kuhusu miradi yake ya silaha.