1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
BiasharaKenya

EU na A. Mashariki kuboresha zaidi upatikanaji masoko, Ulaya

6 Oktoba 2023

Umoja wa Ulaya kwa kushirikiana na Jumuiya ya Afrika Mashariki, zimezindua rasmi awamu ya pili ya mpango wa kuboresha upatikanaji masoko kwa wafanyabiashara wadogo barani Ulaya.

https://p.dw.com/p/4XCXc
Mpango wa kuimarisha masoko utahusisha pia bidhaa za matunda ya parachichi na nyinginezo
Mpango wa kuimarisha masoko utahusisha pia bidhaa za matunda ya parachichi na nyinginezoPicha: M. Afzal

Mpango huo wa kuboresha upatikanaji masoko kwa wafanyabiashara wadogo barani Ulaya, unajulikana kama MARKUP II na utagharimu yuro milioni 40. 

Katika uzinduzi wa mpango huo uliofanyika makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Arusha Tanzania, Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini humo Christine GRAU, pamoja na mambo mengine amebainisha kwamba dhamira ya Umoja wa Ulaya ni kusaidia makampuni ya Afrika Mashariki kupanuka kibiashara na kutoa ajira kwa vijana.

Kulingana na Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dr. Peter Mathuki, awamu hii ya pili itawajumuisha wanawake na vijana katika biashara, huku wizara husika kutoka serikali za nchi wanachama zikitarajiwa kutoa mwelekeo wa jumla wa kuendesha mpango huo, unaotoa kipaumbele kwa mazao ya kilimo kama vile Parachichi, Kakao, maharagwe na Chai.

Awamu ya kwanza ya mpango huo iliyanufaisha takribani makampuni 700 ya kikanda na kuwezesha upatikanaji wa Dola zaidi ya milioni 10 za kimarekani.

Sikiliza pia:

Ushawishi wa kilimo cha parachichi Nakuru