1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moto wa nyika wasababisha vifo vya watu 55 Marekani

11 Agosti 2023

Moto wa nyika uliozuka huko Maui, Hawaii umesababisha vifo vya watu 55 na inaelezwa kuwa idadi hiyo inaweza kuongezeka.

https://p.dw.com/p/4V2RV
Eneo lililoharibiwa kwa moto Hawaii
Moto uliozuka huko Hawaii umesababisha uharibifu usio kifani wa mali na maisha ya watuPicha: Rick Bowmer/AP Photo/picture alliance/dpa

Maafisa wa Hawaii wamesema moto huo ni miongoni mwa majanga mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika historia ya jimbo la Marekani. Kwa mujibu wa maafisa wa Kaunti ya Maui, maafisa wa zima moto wanaendelea kupambana kuuzima moto huo.

Rais wa Marekani, Joe Biden ametangaza moto huo kuwa janga kubwa na kuidhinisha msaada wa shirikisho kwa ajili ya shughuli za uokozi na kiutu.

Moto huo unafuatia matukio mengine mabaya ya hali ya hewa Amerika ya Kaskazini wakati wa majira ya sasa ya joto, huku mioto ya nyika iliyovunja rekodi ikiwa bado inawaka Canada na wimbi kubwa la joto linaloikumba sehemu ya kusini magharibi mwa Marekani.

Ulaya na maeneo mengine ya Asia pia yameshuhudia kupanda kwa viwango vya joto.